Google PlusRSS FeedEmail

NEY WA MITEGO KWENDA KIMATAIFANyota wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Nay wa Mitego amesema kuwa amejipanga kufanya collabo na msanii kutoka nchini Nigeria ili aweze kuutangaza muziki wake katika soko la kimataifa.

Nay amesema kuwa mpaka sasa ameshaandaa bajeti ya milioni 60 kwa ajili ya kufanikisha kufanya collabo na msanii kutoka nchini Nigeria japo mpaka sasa hajajua ni nani atafanya nae collabo hiyo.

Nay ameongeza kuwa gharama hizo itakuwa ni pamoja na gharama za video ambayo anatarajia kuifanya nchini Afrika Kusini na muongozaji mahiri Afrika. GodFather au kwa kumsafirisha muongozaji wake Kevin Bosco.

Aidha Nay amesema kuwa kufanya collabo si gharama ndogo ni lazima mtu ujipange hivyo yeye tayari ameshajipanga vya kutosha kilichobaki ni kufanya collabo tu kwani anaamini milioni 60 inatosha kukamilisha zoezi hilo.

Katika hatua nyingine, video ya wimbo wake ‘Akadumba’ wa Nay wa Mitego bado unafanya vizuri katika soko la muziki kituambacho kinazidi kumpa moyo wa kulivamia soko la kimataifa kwa nguvu zote.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging