Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WA FILAMU WAUNGANA KUPIGA VITA MAUAJI YA ALBINO

Wasanii wa sinema za Kibongo, Jacob Steven 'JB' alijikuta akiungana na mastaa wenzake, Amri Athumani 'Mzee Majuto' na Single Mtambalike 'Richie' walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1) aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa vibaya kichwani, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.

Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani hapa ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo aliyetekwa mjini Geita hivi karibuni.

Walipofika wodini hapo, JB na wenzake walitoa yao ya moyoni kupinga vikali ukatili aliotendewa mama huyo na mwanaye huku wakitahadharisha juu ya laana inayoweza kuikumba jamii yetu kwa tukio hilo.

JB: Nampa pole sana mama Yohana. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na jamii pana duniani.
Watu hawafanyi kazi kujipatia kipato halali. Mafisadi wanataka kujipatia fedha kupitia njia za kishetani za kuwaua wenzetu. Albino ni wenzetu na tunawapenda. Lazima wahalifu wakamatwe na wahukumiwe kunyongwa.


Mzee Majuto: Inasikitisha sana. Haivumiliki. Albino ni wenzetu na wana uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa letu. Wahusila lazima wakamatwe na tuone wakichukuliwa hatua kali.Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.Mara baada ya mastaa hao kutoa la moyoni katika wodi aliyolazwa mama huyo, iligeuka kama msiba kwani kila aliyekuwepo alikuwa akiangua kilio kwa uchungu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging