Google PlusRSS FeedEmail

JAY DEE AKERWA KUZUSHIWA MIMBA


Mwanamuziki nguli wa kike hapa Tanzania Lady JayDee ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Forever amefunguka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya mashabiki wake wa Instagram ambao walimuelewa vibaya baada ya kupost picha jana na kusema kuwa tumbo lake limevimba baada ya kupata msosi wa maana na mzuri.

"Imebidi nifute post Ili nielezee upya.Hivi watu hamuelewi kiswahili au ni nini ??? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani,nikimaanisha mlo na nili post nakula hapo awali Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakayewatoa katika shida zote mpaka mnishikilie mimba mimba..Hebu niacheni basi khaaa Nisiishi Kisa mimba? Aisee mnaboa sana. Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee kero kabisa." aliandika Jide

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging