Google PlusRSS FeedEmail

MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA MARVIN GAYE KULIPWA FIDIA YA DOLA MILIONI 7.3

Mahakama nchini Marekani imetoa uamuzi kuwa mwandishi wa wimbo wa Blurred lines, ambayo ni singo iliyouza mno, aliiba mashairi ya wimbo wa Marvin Gaye.

Jopo la wazee wa mahakama Jijini Los Angeles limesema singo hiyo ya mwaka 2013 iliyoimbwa na Pharrell Williams na Robin Thicke imevunja sheria za hati miliki kwa kuiba mashairi ya wimbo Got To Give It Up wa Gaye alioutoa mwaka 1977.

Kutokana na kosa hilo mahakama imeamuru familiya ya marehemu Mravin Gaye, kulipwa dola milioni 7.3 kama fidia.

Hata hivyo Thicke na Williams wamekanusha kuiga traki hiyo kali na wakili wao amesema uamuzi huo wa mahakama ni wa kutisha.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging