Google PlusRSS FeedEmail

KAZI KUBWA KULINDA HESHIMA YANGU- NISHA


                             


MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu na Komedi Salma Jabu ‘Nisha’ amedai kuwa ana kazi kubwa katika kulinda nafasi yake ya uigizaji bora wa Komedi na ustadi katika kutengeneza kazi zake na ziendelee kuwa bora ili asipotee na kuonekana kama alibahatisha.

 “Wahenga husema kuwa ni rahisi kupata nafasi ya kwanza, lakini si rahisi kuilinda hivyo name lazima niilinde nafasi yangu niliyoipata mwaka jana baada ya kuipigania kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu na nitailinda kwa kufanya kazi bora tu,”anasema Nisha.

          

Msanii huyo anaamini kuwa kwa Bongo si kazi nyepesi kufanya kazi na kukubalika na wapenzi wa filamu kwani kila siku wasanii wanaongezeka na kuja katika hali ya ushindani mkubwa ambao kama haujajipanga lazima upotee katika tasnia ya filamu baada ya kuvuma kwa muda mfupi tu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging