Google PlusRSS FeedEmail

RAY - SIKURUPUKI KUTENGENEZA FILAMU

                         

MWIGIZAJI Nyota na muongozaji wa filamu mahiri katika tasnia ya filamu Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ amefunguka kwa kusema kuwa sinema zake si kuangalia filamu gani imeingia sokoni na kufanya vizuri kwa staili fulani na yeye akakurupuka na kutengeneza filamu kwa mlipuko.

“Mara nyingi wapenzi wa sanaa si rahisi wanapenda nini? Lakini ninawajua wapenzi wa filamu zangu hivyo inakuwa vigumu sana kujiingiza katika filamu za mlipuko, baada ya filamu moja kufanya vizuri, basi kila mtu anatoka na staili hiyo hiyo,”anasema Ray.

“Tumeshuhudia filamu kama Chausiku, na nyinginezo zilizotengenezwa katika maandhari ya maisha yetu mitaani basi kila sinema ni hivyo hivyo, ni wazi inaonyesha kuwa hatuamini mawazo yetu,”anasema Ray.

Ray anasema kuwa ukitengeneza filamu ya msimu pia msimu ukiisha watu wanaisahau na kuendelea sinema nyingine lakini pia wapenzi wa filamu Swahilihood hawataki kubwa zilizotengenezwa kwa akili nyingi, akatolea mfano wa sinema ya Crazy ya marehemu Kanumba haikufanya vizuri.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging