Google PlusRSS FeedEmail

SEKI NA JOTI WAKANUSHA UVUMI WA KIFO CHA VENGU

BADO hali ya uvumi katika mitandao ya kijamii inaendelea huku kuvumishwa kwa vifo kwa baadhi ya wasanii, ambapo hivi karibuni imezuka story ambayo imeenea sana mitandao ya kijamii na pia watu wamekuwa.

 wakitumiana PICHA Whatsapp na wengine wameweka pia kwenye kurasa za Instagram na kuandika #RIP inayomuonesha picha ya mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba aka Vengu ambaye ni muda mrefu hajaonekana akiigiza pamoja na kundi lake baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Seki ambaye ndiye muongozaji wa kundi hilo amekanusha kwa taarifa hzo na kudai kuwa ni taarifa za uongo ambazo zimeenezwa na watu wazushi.

Wakizungumza na Clouds FM muda mfupi uliopita Seki pamoja na Joti wameeleza wazi kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging