Google PlusRSS FeedEmail

ANGELINA JOLIE ATOLEWA KIZAZI
Muigizaji Angelina Jolie amelazimika kutoa mishipa ya kupitisha mayai na vifuko vya mayai baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.

Muigizaji huyo maarufu wa Hollywood ameidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa uzazi wake juma lililopita katika upasuaji wa dharura.

''Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani'' alisema Bi Jolie

Habari hizi zimewashtua wafuasi na mashabiki wa totoshoo huyo ambaye miaka miwili tu iliyopita alilazimika kukatwa matiti kwa sababu ya tishio hilohilo la Saratani.

Aidha mama wa  muigizaji huyo nyota aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.

''Sio jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu'' alisema Jolie.

Jolie ambaye ni mumewe ni  muigizaji nyota wa Holywood  Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.

Wawili hao wana   watoto sita. na Mamake tayari aliaga Dunia kutokana na Saratani

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging