Google PlusRSS FeedEmail

TYGA AVUJISHA NYIMBO YA MINAJ

HATIMAYE Rapa Nicki Minaj ameamua kuweka wazi chanzo cha kutokuelewana na msanii mwenzake Tyga huku ikitajwa kuvujisha nyimbo ndio sababu ya kuwepo kwa tofauti hizo baina ya wawili hao.

Ambapo Minaj ameweka wazi tofauti zao na kusema kuwa tofauti hizo ziliibuka mara baada ya  rapa Tyga alipovujisha wimbo wake wa “Truffle Butter” sauti yake ikiwemo.

Nicki anasema awali Tyga, Drake na Lil Wayne walitakiwa kuwepo kwenye wimbo huo ila sauti za Tyga zilitolewa na uongozi.

Nicki Minaj anasema Tyga alimuomba msamaha kuhusu kauli zake kuwa Nicki Minaj ni mbinafsi na hajawahi kumsaidia sababu ni uongo, Nicki Minaj aliwahi kumpeleka Tyga kwenye ziara zake zote za Uingereza kabla Tyga hajawa msanii mkubwa.

Nicki anasema Tyga alinitumi sms kuomba msamaha nika msamehe tu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging