Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WAGOMEA KUTUMIKA KATIKA KUPIGIA DEBE KATIBA MPYA

           

Katika hali ya kuonyesha kuwa wasanii nchini wameanza kujitambua, leo hii walimgomea Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo alipotaka wawe mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kuiunga mkono katiba pendekezwa.

Wakionekana kuchoshwa na hali ya kutumiwa na wanasiasa kutimiza malengo yao ya kisiasa na kisha kuwabwaga, wasanii na viongozi wao wakiongozwa na Asha Baraka, mkurugenzi wa ASET.


Walitumia fursa ya kuuliza maswali kutoa yao ya moyoni huku wakiweka bayana kuwa sanaa ni ajira yao hivyo wao wanaangalia soko linataka nini na kama serikali itataka waifanye kazi hiyo basi serikali itoe ruzuku ili hata wasanii hao wakikosa soko la kazi hizo za kupigia debe katiba wasiingie hasara.

Pamoja na Waziri na viongozi wengine kutumia lugha tamu ya kutaka watu wawe wazalendo kwa kutoa mifano ya wasanii wa zamani, wasanii walikiri kuwa wao ni wazalendo ila sanaa ni ajira yao.

Na walienda mbali zaidi kwa kubainisha kuwa wasanii wa zamani walikuwa wameajiriwa na taasisi mbalimbali za serikali kama UDA, Bima, Magereza nk lakini wao sasa hivi wamejiajiri katika sanaa, ilikuwa rahisi kutunga nyimbo za hamasa kuhusu tukio la Serikali.

Wasanii wanaamini kuwa suala la kampeni limekuwa na fungu lake hivyo hakuna sababu ya kuwaomba wasanii wapige kampeni kwa kujitolea wakati maslahi yao hayajabaishwa wazi ni suala la Kitaifa kila mtu aipigie kura katibu kwa uelewa wake.

Swali linakuja kuna wimbo ulizinduliwa Dodoma na ulishirikisha wasanii wengi wa Bongo Fleva kampeni ile waandaaji hawakulipwa? Wasanii wanaoangaliwa sana kwa sasa ni muziki na filamu na hawa ndio hasa wanatakiwa kutumika.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging