Google PlusRSS FeedEmail

BABAAKE KIM KARDASHIAN SASA NI MWANAMKE ?Bruce Jenner aliyekuwa mwariadha bora duaniani kabla ya kuwa nyota wa kipindi cha televisheni na familia moja maarufu duniani ''The Kardashians''. sasa amefichua siri ambayo amekuwa akiificha kwa miaka mingi.

''Kwa nia na madhumuni yote, mimi ni mwanamke.'' Jenner aliambia Sawyer kutoka ABC katika mahojiano maalum yaliopeperushwa hewani siku ya Ijumaa.

''Watu wananiona tofauti,wananiona kama mwanaume, lakini moyo na roho yangu na kila kitu ninachofanya maishani ni sehemu yangu.'' Jenner ambaye ana umri wa miaka 65 amesema. '' Upande huu wa kike ni sehemu yangu. hivi ndivyo mimi nilivyo.''

Katika masaa ya mahojiano na Diane Sawyer mjini New York na California, Jenner alielezea kwa kina mapambano yake ya kuwa na jinsia mbili tangu utotoni.

''Akili zangu ni za kike sana kuliko za kiume.'' Ameongezea. '' Ni vigumu sana watu kuelewa, lakini hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyo.''

Jenner aliyejawa na hisia na mwenye nywele ndefu shati na suruali ndefu alisema kuwa amesubiri kwa miaka mingi ili kujitangaza kwa kuwa hakutaka kuwavunja moyo watu.

Kwa miongo kadhaa wake wa zamani wa Jenner na madada zake waliweka siri kuhusu jinsia yake na kwamba walikuwa watu waliokuwa wakijua siri hiyo.

Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo ulipanuka hivi majuzi wakati Jenner alipomwambia mamaake na wanawe 10 .

Jenner ana watoto sita Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na Kylie pamoja na watoto wanne wa kambo akiwemo Kourtney,Kim,Khloe na Rob Kardashian.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging