Google PlusRSS FeedEmail

MUIGIZAJI WA FILAMU ZA KINAIJERIA ASHINDA UBUNGEMuigizaji maarufu kutoka Nollywood, Desmond Elliot ameshinda uchaguzi katika kuwakilisha jimbo lake la Surulere 1 katika Lagos State Assembly.

Desmond aliyegombea kwa tiketi ya chama cha All Progressive Congress(APC), alipata kura 23,141 na kumshinda Bayo Smith wa PDP aliyepata kura 12,546. Katika ukurasa wake wa Facebook Desmond aliwashukuru waliompigia kura na kuahidi kutimiza ahadi zake. 

Chama cha APC pia kimeshinda asilimia kubwa ya viti vya Magavana kwa kushinda vit 19 kati ya 28, ukijumlisha na kuwa katika uongozi wa juu APC pia kimechukua Urais wa nchi kupitia Muhammadu Buhari,Nigeria imekuwa nchi ya APC, hili limekuwa ni pigo jingine kubwa kwa chama tawala kilichokuwa madarakani toka serikali ya kijeshi ilipoondoka madarakani 1999 mapinduzi yalipoisha 

 Rais Buhari ataapishwa tarehe 29 May.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging