Google PlusRSS FeedEmail

RIYAMA AMTULIZA WEMA SEPETUWiki iliyopita mashabiki na followers wa Wema Sepetu, walipatwa na sintofahamu baada ya bi shost huyo kuandika mambo mazito kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

CEO huyo wa Endless fame aliandika ujumbe mzito kuhusu tatizo linalomsumbua la kutoshika ujauzito. Wema alifunguka yafuatayo

“Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningezaamuda mrefu sana but sina…. na siwezi kumkufuru mwenyezi mungu katika hili, au mngependa niwaambie jinsi ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe? Is da twat yu want? Au mnafikiri siumii mnavyonisema kuhusu kupata mtoto? Kiukweli nahangaika sana juu ya tumbo langu ili kupata mtoto” aliandika Wema

Watu wengi waliguswa na ujumbe wa Wema, kila mmoja alijaribu kuonesha hisia zake juu ya waraka huo miongoni mwao akiwamo staa wa kike anayefanya vizuri kwenye kiwanda cha filamu bongo Riyama Ally.

Staa huyo alitenga muda wake juzi kwa ajili ya kumuandikia ujumbe Wema Sepetu ili kumpa faraja katika kipindi hichi kigumu anachopitia, Riyama amesema Wema hana budi kulikabidhi swala hilo kwa mwenyezi mungu kwakuwa yeye ndio ajuae shari na kheri za mja wake.

“Naomba hapa unisikilize kwa makini, nabii Ibrahim alimpata nabii Ismail akiwa na umri mkubwa sana (utuuzimani) wema bado mdogo muda utafika inshaalah mola atakupa mume mwenye heri na uzae jike na dume, usijali mama mungu hukupa akujalialo si umuombalo watoto ni kudra za mola na sio jitihada za wanaadama” aliandika Riyama kupitia Instagram

Kauli ya Wema inakuja baada ya Diamond kufunguka kuwa wasichana wote aliokuwa nao kwenye mahusiano kabla ya Zari hawakuwa tayari kupata nae mtoto.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging