Google PlusRSS FeedEmail

WASANII KUVIMBA VICHWA KUNAUA SINEMA- MBEMBE

                                  

SEIF Mbembe mwigizaji mkongwe anayetamba katika tasnia ya filamu  anachukizwa na tabia za baadhi ya wasanii kufika sehemu za kazi na kutumia muda mwingi kuchezea simu na kuwachelewesha wasanii wengine ambao wanakuwa wapo kwa ajili ya kazi na si ubishoo unaofanywa na wasanii wenye majina makubwa.

“Kinachotukutanisha pale ni kazi sasa mtu mwingine anavyoleta utoto na ni mtu mzima haipendezi, wanadharau sana hasa wakiitwa masupa star vichwa vinavimba sana, lakini bila nidhamu katika kazi ni sawa na bure, ndio maana hakuna msanii anayejiita star anafanya kazi na wazungu,”anasema Mbembe.
Msanii huyo amesema kuwa moja ya sifa kubwa ya msanii ni kujiheshimu pamoja na kuheshimu kazi unayotakiwa kufanya na si vinginevyo lakini si wasanii wenye majina wa kibongo ambao wanajua wajibu wao wakiwa kazini jambo ambalo linasababisha tasnia ya filamu kushindwa kusonga mbele kwa kukosekana nidhamu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging