Google PlusRSS FeedEmail

BI.CHEKA ATANGAZA NAFASI YA UCHUMBA, YUPO TAYARI KUOLEWAKama wewe ni mwanaume na unahitaji mke nafasi hii hapa, Msanii mkongwe nchini Bibi Cheka amewaka wazi kwamba endapo atatokea mwanaume wakapendana kwa dhati yupo tayari kuolewa!

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bi. Cheka alisema yeye kama mwanamke anasifa na vigezo vyote vya kuwa na mume wa mtu.

“Nimewahi kuolewa na nilibarikiwa kuzaa watoto tisa lakini baadae tuliachana na mume wangu kutokana na ulevi,” anasimulia Bibi Cheka.

Bibi Cheka aliendelea kusema kwamba, tangu hapo hajaolewa tena lakini kwa sasa kama atatokea mtu wa kumuoa yupo tayari ingawa alipoulizwa kuhusu umri wake bibi huyo alisema hakumbuki mwaka aliozaliwa wala miaka yake!

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging