Google PlusRSS FeedEmail

BILL COSY ALIKUWA AKIWALIPA WANAWAKE FEDHA BAADA YA NGONO


                               

Msanii wa vichekesho nchini Marekani Bill Cosby amekiri kujaribu kuwalipa wanawake aliofanya nao tendo la ngono kulingana na ushahidi uliopatikana na gazeti la the New York Times kwa lengo la kuwanyamazisha.Gazeti hilo linasema kuwa bwana Cosby alitoa ushahidi huo miaka 10 iliopita.

Kesi hiyo ilianzishwa na mfanyikazi mmowa zamani wa chuo kikuu mjini Philadelphia ambaye alidai alimpatia dawa za kulevya na baadaye kumnyanyasa.Bwana Cosby mwenye umri wa miaka 78 anakibiliwa na msururu wa mashtaka ya unyanyasaji.

Hatahivyo amekana madai hayo.Ushahidi wa kortini uliofunguliwa mwezi huu umeonyesha kuwa alikiri kuwapatia dawa za kulevya wanawake kwa lengo la kutaka kufanya ngono nao.

Bwana Cosby alihojiwa kwa siku nne mwaka 2005 na 2006 katika hoteli moja ya Philadelphia.Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Andrea Constand,aliyekuwa mfanyikazi wa chuo kikuu cha Temple,chuo ambacho bwana Cosby alikuwa na uhusiano nacho wa karibu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging