Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND "SINA HAJA YA KUSHINDANA NA WATU"Siku chache baada ya kuibuka na tuzo za MTV kipengele cha Mtumbuizaji Bora Afrika msanii Naseeb Abdul a/k/a Diamond Plutnumz amesema yeye yupo kwa ajili ya kuufikisha muziki wake ufike mbali na sio kuisndana na mtu.

Diamond alisema hayo jumatatu ya july 20. 2015 wakati akipiga stori na mtangazaji Jabir Salehe ndani ya kipindi cha The Jump Off ndani ya Timesfm,

“Mimi nishafuta swala kufanya muzik kushindana na mtu hususani tena kwa msanii wa hapa nyumbani, nimeshafanya mambo mengi, nimechukua tuzu kibao nyumbani,huu sio muda wa wasanii watanzania kuonyeshashana ubabe, kinachotakiwa ni kupambana kufanikisha muziki wetu unavuka mipaka ”.

Diamond aliendelea kwa kumpongeza msanii mwenzake Vanessa Mdee kwa mara ya kwanza kuingia kwenye tuzo za MTV, huku akiamini kwamba mwanadada huyo atachukua tuzo mojawapo mwakani kama akiendelea na juhudi zake anazozionyesha.

Diamond pia amewaomba wataznzania kuanza kupiga kura kwa wasanii wote waliochaguliwa kuingia kwenye tuzo za Afrimma ambap wasanii saba toka nchini Tanzania.

Wasanii hao ni yeye mwenyewe DiamondPlutnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Mrisho Mpoto , Lady Jaydee, Ommy Dimpoz na Khadija Kopa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging