Google PlusRSS FeedEmail

BOBBI KRISTINA AFARIKI DUNIA

                      

Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.

Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.

Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''.

Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa.

Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging