Google PlusRSS FeedEmail

DRAKE NDANI YA REMIX YA WIMBO WA WIZKID

Ni wazi sasa game ya muziki wa Afrika inazidi kupaa na kuvuka mipaka na hii ni kutokana na muziki huo kupata airtime kwenye vituo mbalimbali vya vyombo vya habari hususani bara Ulaya na Amerika.

Baada ya P Squre kufanya kazi na Wanamuziki wakubwa kama Akon na Rick Ross, sasa msanii mwingine anayetikisa anga la muziki Afrika kutoka huko Nigeria Wizkid amefanya remix ya wimbo wake wa Ojuelegba na rapa Drake.

Wimbo huo kwa mara ya kwanza ulisika ukichezwa hewani kwenye kituo cha radio cha OVO Sound siku ya jumamosi wakati Drake akifanyiwa mahojiano kwenye radio hiyo.

Pia katika wimbo huo imesikika sauti ya rapa kutoka uingereza Skepta a/k/a Skeppy.

Bila shaka hii itakua hamasa kubwa kwa wasanii wengine barani Afrika kuhakisha wanafanyakazi kwa juhudi kubwa ili kuweza kuutangaza muziki toka bara la Afrika sehemu nyingi duniani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging