Google PlusRSS FeedEmail

JOKATE AMLALAMIKIA DIAMOND, ADAI KUMCHONGANISHA NA ALI KIBA



Hii inakuja Baada ya kushinda tuzo ya Best Act kwenye tuzo za Mama [Mtv AFrika Music Awards], mkali wa Bongo fleva Diamond Platnumz aliweka video ikimuonyesha aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Jokate akicheza na kufurahia wimbo wake.

Video hiyo imeonekana kama kumdhalilisha Jokate sababu ya Ukaribu wake na anayeaminiwa kuwa hasimu wa Diamond Platnumz Ali Kiba. Haya maneno ya Jokate baada ya video hii kuonekana kwenye social Networks.

“Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni #TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukuma akani-record na kumtumia @diamondplatnumz bila mimi kujua. Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi kucheza mziki wowote uupendao.

Ila kitendo cha @diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi 1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa kwa taifa ila 2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe nani?

Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficial anatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life 3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanaweke aliokuwa nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu dangote.

Which to me is just dead wrong. @diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi kutugeuka. Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo.

Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila @babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo? Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.” Ameandika Jocate.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging