Google PlusRSS FeedEmail

NICKI MINAJ NA LIL WAYNE NDANI YA JUKWAA MOJAPamoja na kila mmoja kuonekana kufanya mambo yake, huku kundi walilokuwawakifanyakazi pamoja YMCB kusimama kutokana na mgogoro wa wasanii na uongozi mzima wa kikundi hicho, lakini sio sababu ya Mwanahiphop bora wa kike nchini Marekani na rapa mwenye style nyingi Lil Wayne kuendelea kuheshimiana na kupendana.

Jumapili ya july 26 Nicki Minaj alikuwa kwenye mji wa Brooklyns ndani ya ukumbi wa Barclays Center ambapo alikuwa anapiga show yake ya kuitangaza project yake ya Pinkprint.

Nicki alisimamisha performance yake na kufanya surprise kwa mashabiki waliofurika kwenye ukumbi huo kwa kumuita Lil Wayne jukwaani. Mashabiki wapaza sauti za juu za furaha walipomuona Lil Wayne ambaye aliperfom nyimbo kadhaa zikiwemo Royal, A Milli na 6 Foot, 7 Foot.

Kabla ya Lil Wayne a/k/a Lil Weezy kuimba, mwanadada Nicki Minaj aliueleza uma ulifurika ndani ya ukumbi huo kwamba anamkubali sana brother wake huyo, na Lil Wayne ndiye aliyefanya mpaka Nicki kuwa juu na kubadilisha maisha yake.

Lil Wayne naye hakusita kupokea shukrani hizo na kujibu kwamba hata Nick anamchango mkubwa kwenye sanaa ya Lil Wayne.

Bofya Hapa ucheck kipande cha Video Nick alivyomkaribisha Lil Wayne kwenye show yake https://www.youtube.com/watch?v=YOGFpB0Jedg

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging