Google PlusRSS FeedEmail

CELINE DION APOKEA NYIMBO 4000 HUKU AKIENDELEA KUMUUGUZA MUMEWE

MWANAMUZIKI ambaye ni staa  wa RnB, Celine Dion ambaye ameshindwa kuendelea na kazi yake ya muziki vizuri kutokana na hali mbaya ya kiafya ya mume wake anayeugua saratani ya kooni, ameripoti kuwasilishiwa nyimbo 4,000 baada yake kutangaza anahitaji kuandikiwa wimbo mpya.

Ombi lake Dion la kuomba wimbo kwa ajili ya albamu yake mpya ya Kifaransa lilipokelewa kwa uzito mkubwa kinyume na matarajio yake, ikiwa ni baada ya kuwasilishiwa nyimbo chungu nzima kupita maelezo, ambazo zitampa mtihani kuchagua ni upi atakaoingia studio kuurekodi.

Kulingana na kampuni inayomsimamia Dion, takriban nyimbo 4,000 zilikuwa zimetumwa kwenye tovuti yake hadi kufikia wiki juzi huku maombi hayo yakizidi kupokelewa.

Mume wa Dion, Rene Angeli aliyestaafu kuwa meneja wa mkewe kutokana na hali yake ya kiafya pamoja na Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo ya Les Feeling Production, Aldo Giampaolo walielezea kushangazwa na ukubwa wa mwito huo.

Mapema mwezi Agosti, Dion alitangaza kuwa anapokea wimbo mpya kutoka kwa watunzi na kwamba yeyote mwenye kipaji vilevile angeweza kushiriki kwenye mchakato huo wa kumtungia wimbo na matokeo yake ndio kama hayo.

Ombi la Dion ambaye ni raia wa Canada anayeishi Marekani, lilitokana na mkakati wake wa kuhakikisha albamu yake ya Kifaransa inatoka 2015 huku nyingine ya Kiingereza ikitazamiwa kutoka 2017. Kumbuka nyimbo zote hizo alizopokea zipo katika lugha ya Kifaransa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging