Google PlusRSS FeedEmail

RICH MAVOKO HAJUTII KUJIUNGA NA KAKA EMPIRE

MKALI wa muziki wa Bongo Flava nchini , Rich Mavoko aliyesainishwa mkataba na kampuni ya rapa wa Kenya, Rabbit, Kaka Empire amesifia kampuni hiyo kwa kumzidishia shoo zinazompa zinazomuongezea kipato nchini Kenya tangu aliposaini mkataba huo miezi mitatu iliyopita. 

Mwanamuziki huyo anayejisifia kutokana na mkataba huo kutoka kwa  Kaka Empire; dili ambayo hajutii kabisa kiasi kwamba ameamua kuwashauri wasanii wenzake kutumia fursa pindi waipatapo.

Mavoko amewaambia wasanii wenzake kwamba kuna umuhimu mkubwa sana kwa msanii kuwa na wakala kwenye nchi nyingine ambako kazi zao zinafanya vizuri, kama alivyo yeye, ili kurahisisha usimamizi wa kazi zao, hatua ambayo itahawahakikishia mapato.

Rich Mavoko alisaini katika lebo ya Kaka Empire yapata miezi miwili imepita mwaka huu wa 2015 ambapo ukusanyaji wa pesa zinazotokana na mauzo ya muziki wake nchini pamoja na kutafutiwa shoo za hapa Kenya zitafanywa na kampuni hiyo kwa niaba yake.

“Kuna umuhimu kwa wasanii kama sisi Watanzania ambao wengi wao tunaamini kwamba kazi zetu hufika mbali. Kwa hiyo unatakiwa uwe na mtu anayefuatlia kazi zako. Ukiwa na wakala kule nje, inakua rahisi watu kukupata na hata usimamizi wa kazi zako neje unakuwa upo sawa. Kwa mfano mimi nimekuwa nikifanya shoo nyingi Kenya kwa sababu ya wale jamaa (Kaka Empire) akaiambia EATV.

“Mkataba wangu na Kaka Empire wa Kenya wao ni mawala tu wa kule na wala sio mpaka Tanzania. kazi yao ni kutafuta shoo na dili zinginezo wanipe mimi nikafanye. Na hii ndio sababu wiki moja nipo Dar, wiki ya pili niko Nairobi mara Mombasa kwa sababu ya kufanya kazi nao,” akaongeza.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging