Google PlusRSS FeedEmail

PREZZO AWASHTUA MASHABIKI WAKE ISTAGRAM

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Rapa wa siku nyingi ambaye kawa kimya sana kiasi kuwa imebakia kidogo asahaulike, CMB Prezzo kawashtua sana mashabiki wake na kitu alichokifanya hivi karibuni.

Wala sio ngoma mpya aliyoachia, hapana. Ni ile picha aliyoiweka kwenye Instagram hivi majuzi ndiyo iliyozua minong’ono kiasi cha haja miongoni mwa mashabiki wake walioingiwa na mchecheto.

Kwa muda sasa kumekuwepo na tetesi kwamba Prezzo ambaye kipindi cha chuma alikuwa na tabia ya kuringisha mali na pesa zake, sasa jamaa kachacha , yaani kafilisika na hana kitui kabisa.

Taarifa hizo zilizidi kudai kwamba Prezzo kaishiwa kiasi kwamba karudi nyumbani kwa mamake baada ya kushindwa kuendelea kujisimamia kwake.

Tetesi hizo huenda zikanogeshwa hata zaidi na picha yake ya hivi majuzi kwenye Instagram inayomwonyesha msanii huyo akiwa mwembamba sana kupita maelezo ishara tosha kuwa kapoteza kilo nyingi sana.

Hii sio kawaida kwa mashabiki wa Prezzo ambao wamemzoea kumwona akiwa jitu lenye miraba minne ila kwa picha hiyo, mawazo ya haraka kwa wengi huenda pengine wakadhania jamaa alikuwa au anaugua maradhi fulani au kupoteza uzito huo kumetokana na msongo wa mawazo.

Haya ni baadhi tu ya mawazo ya mashabiki wake ambao wamekuwa bize kumhoji mbona kapoteza uzito kiasi hicho. Tangu alipoiwakilisha taifa kwenye shindano la Big Brother Africa miaka mitatu iliyopita na akamaliza katika nafasi ya pili, Prezzo amekuwa akiishi maisha ya ukimya sana bila ya kujishughulisha zaidi na masuala ya muziki kama ilivyokuwa zamani

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging