Google PlusRSS FeedEmail

SHAMBULIZI LABADILISHA MAISHA YA MSANII CARA

HANA haja ya kufahamika tu kwa urembo wake bali anataka kipaji  chake kimuziki iwe kitambulisho chake miongoni mwa mashabiki.  Kutana na Cindy Abila msanii aliyeamua kubadilisha jina lake la usanii kutoka Cindy hadi Cara baada ya kushambuliwa.

Tukio hilo lilitokea mwaka wa 2012 na kusema kweli sipendi kulizungumzia lakini la hakika ni kuwa japo ulikuwa mkasa mbaya, baada ya hapo nilibadilika na kuimarisha ndoto yangu kama mwanamuziki. Kadhalika nilibadilisha jina kama mbinu ya kupata kitambulisho kipya na kuuza muziki wangu upya,” aeleza.

Kufikia sasa ana vibao vitatu ambapo amemakinika kwa mtindo wa RnB Afro Pop huku mada kuu ya nyimbo zake ikiwa kutia moyo na masuala ya mapenzi. Anasema muziki ni mwito ambapo alianza kuimba mwaka wa 2007 na kufanya kibao chake cha kwanza Street love.

“Wimbo Street Love unazungumzia masaibu yanayowakumba vijana mtaani. Kibao hicho kilifuatiwa na KatiKati, wimbo unaonyesha jinsi wapenzi wawili wanaofanya juhudi kuhakikisha uhusiano wao unadumu,” aeleza.

Mbali na hayo ameshirikiana na wanamuziki mbali mbali nje na hapa nchini ambapo mwaka jana pamoja na wasanii tofauti waliangusha wimbo, Safer City, unaozungumzia umuhimu wa kudumisha usalama mitaani.

Japo bado hajang’aa kimuziki anaamini uaminifu na bidii kama nguzo ya ufanisi katika uga huu, tofauti na mtazamo wa wengi kuwa sharti nyimbo na video ziwe na lugha chafu, vile vile mabinti wanaocheza muziki wakiwa nusu uchi.

Ari yake kung’aa kimuziki imechangiwa na wanamuziki kama vile malkia Yvonne Chaka Chaka, marehemu Whitney Houston, Mariah Carey na Beyonce miongoni mwa wengine.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging