Google PlusRSS FeedEmail

MWIGIAJI BRENDA WAIRIMU AKOSA FURSA ADIMU YA KUFUZU HOLLYWOOD

HUWA kuna aina mbili ya bahati; bahati mbaya na bahati nzuri. Iliyomkuta mwigizaji Brenda Wairumu ni bahati mbaya licha ya kuwa alipasi majaribio ya awamu ya kwanza ya kipindi cha BET Top Actor Africa ambayo humpa mwigizaji fursa ya kupenyeza Hollywood.

Bahati mbaya ilikuja pale Brenda alitakiwa kushiriki majaribio ya raundi ya pili jijini Johanessburg, Afrika Kusini Ijumaa Oktoba 16, 2015, suala ambalo lilikuwa nzito ikizingatiwa kwamba notisi ya siku moja ilikuwa ya haraka mno!

Staa huyo wa nyumbani kwa sasa hesabu ambazo angelikuwa akipiga ni namna ambavyo angepokelewa Hollywood na Lupita Nyo’ngo miongoni mwa mastaa wengine.

Hii ilikuwa ni baada ya mwigizaji huyo wa kipindi cha ‘Mali’ kupasi kwenye majaribio ya kipindi cha BET Top Actor Africa ambayo inaendelea kuwasaka waigizaji bora kutoka Afrika itakaowasaidia kupenyeza kwenye majaribio ya Hollywood.

Ukiweka wazo hilo la kuigiza Hollywood pembeni kidogo, mshindi wa Top Actor vile vile atatia kibindoni kitita kizito cha Sh1 milioni.

Lakini matumaini ya Brenda kuigiza Hollywood kando na kushinda tuzo hilo sasa yamefifia licha yake kupasi kwenye mchujo wa raundi ya kwanza.

Majaribio hayo ya raundi ya kwanza yalifanyika katika ukumbi wa Kenya National Theatre Alhamisi jijini Nairobi ambapo Wairimu alipasi. Kwenye majaribio ya raundi ya pili, mwigizaji huyo alitakiwa na waandalizi wa shindano hilo kusafiri hadi Johanessburg, Afrika Kusini Ijumaa, suala ambalo lilimuiwa vigumu ikizingatiwa kwamba notisi ya siku moja ilikuwa ya haraka sana.

“Hujambo Brenda, asante kwa kushiriki majaribio yetu ya Top Actor Africa. Umepasi raundi ya kwanza na utatakiwa kushiriki ya pili itakayofanyika Johannesburg katika studio za Urban Brew Ijumaa (Octoba 16),” Ndio ujumbe aliotumiwa wa kumfahamisha.

Lakini kutokana na ugumu huo wa usafiri, washirika wote kutoka nje ya Afrika Kusini waliopasi raundi ya kwanza, walitakiwa kufanyiwa majaribio ya raundi ya pili kupitia mtandaoni lakini baadae mpango huo ukaahirishwa na wote kutakiwa kufika Urban Crew jambo ambalo hangeweza.

“Mashabiki wangu taarifa za kuhuzunisha ni kwamba sitaweza kuhudhuria majaribio ya BT Top Actor. Raundi ya pili ilipaswa kufanyika mtandaoni lakini mambo yakabadilika na nikatakiwa niwe pale.

Kwa notisi ya siku moja kuwa Johannesburg, ni vigumu sana kwangu kusafiri kutokana na notisi hiyo fupi hivyo nimelazimika kuachia nafasi yangu ipotee,” Brenda aliandika kwenye Twitter.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging