Google PlusRSS FeedEmail

ALBAMU YA ADELE KUWEKA HISTORIA MPYA UK

                                

Albamu ya mwanamuziki Adele huenda ikaweka historia nchini Uingereza kwa kuwa albamu iliouza zaidi ,ikiwa tayari imeuza zaidi ya kopi nusu milioni katika kipindi cha siku tatu pekee.

Jumla ya mauzo ya 25 ni kopi 538,000 kufikia sasa ,huku zikiwa zimesalia siku nne za chati hiyo.Ni Albamu mbili pekee zilizouza zaidi ya kopi 500,000 katika juma moja.

Take that Progress iliuza kopi 519,000 katika wiki ya uzinduzi wake mnamo mwaka 2010 na Oasis Be here Now ambayo inashikilia rekodi hiyo ikiuza kopi 696,000 katika wiki yake ya kwanza mwaka 1997.

Wakati huohuo nchini Marekani,Adele amevunja rekodi ya kuuza kopi milion 2.3 za albamu hiyo kufikia sasa.

Mauzo ya takwimu hizo yanathibitisha kwamba huenda rekodi inayoshikiliwa na bendi ya Nsync iliotowa albamu yake mwaka 2000 'No Strings Attached' iliouza kopi milioni 2.4 katika wiki yake ya kwanza ya uzinduzi ikavunjwa.

Adele alicheza single yake Hello siku ya jumamosi.Mziki huo pekee umeuza kopi milioni 2.5 katika kipindi cha wiki nne pekee.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging