Google PlusRSS FeedEmail

MAENDELEO YA FILAMU TANZANIA

                                          Bicco Mathew

WAKATI msemo wa Hapa kazi ukiwa ndio habari ya mjini na sisi tunasema “ FILAMU KAZI” jukwaa la Wanaharakati wa maendeleo ya filamu Tanzania limeundwa na linaendelea kufanya vema kuelekea kutafuta suruhu au dawa ya soko la filamu kwa kuangazia matatizo au changamoto zinazo ikabili tasnia hiyo yenye uwezo wa kuajiri watu wengi pengine kuliko sekta yoyote

Katibu wa JWMFT Bicco Mathew amsema kuwa wadau walikutana katika Hoteli ya Valentino iliyopo Kariakoo kuitikia wito wa Ndg. Myovela Mfwaisa juu ya kuhudhuria kwenye mjadala wa juu ya namna gani tutaisaidia tasnia ya Filamu nchini kupata soko nje ya mipaka ya Tanzania, kuleta hamasa kubwa kwa wadau waliohudhuria katika kikao hicho huku kila mdau akichangia kwa umakini zaidi.

“Hapa mimi naongea kama mwanaharakati pia nitafafanua baadhi ya mambo ambayo inaoneka kama TAFF imeshindwa kufanya lakini ukweli ni kwamba siku zote tunapigania kupata sera ya filamu,”

“Ni kweli kimaandishi Serikali imerasimisha filamu lakini Wizara husika imeshindwa kuonyesha dira ili tasnia ya filamu iweze kupata sera ambayo ndio kitu muhimu sana kwa sasa,”alisema Bicco.

Wajumbe John Kallaghe, Gallus Mpepo walishauri kuwa kuna haja ya wasanii kuhudhuria semina pamoja shule za muda mfupi ili kukabilia na ushindani wa filamu za kimataifa kama legho likiwa kufika katika soko la kimataifa.

Aidha mwigizaji wa siku nyingi Bakary Masasi alisema kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinadumaza wasanii kwa kuwakatisha tama kuwa baada ya kifo cha marehemu Steven Kanumba filamu imeshuka kitu ambacho anasema si kweli bali ubunifu umepotea.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging