Google PlusRSS FeedEmail

HORMINIZE AELEZEA SABABU ZA KUTOONEKANA JUKWAANI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini anayetamba na wimbo wa 'Aiyola' chini ya usimamizi wa WCB, Horminize ameelezea sababu za kutoonekana kwenye majukwaa akifanya show yoyote ile alisema kuwa alitaka kuhakikisha anakamilisha video ya wimbo wake huo unaonekana kupendwa sana na mashabiki wake.

Aiyola ni wimbo wake uliomtambulisha kwenye game ya muziki wa bongo fleva chini ya usimamizi wa WCB Wasafi iliyoko chini ya Diamond Platnumz.

Horminize ambaye kwasasa anafanya vizuri na video yake ya Aiyola aliyoifanya nchini South Africa.Hormize hakusita kuweka wazi sababu zilizomfanya kuchelewa kuonekana kwenye jukwaa.Horminize alisema

”Kuna email nyingi zimeingia za show,lakini kikubwa tulitaka tufanye kwanza video ndio niweze kufanya show,mpaka sasa kuna show nyingi kuanzia Mombasa,Nairobi,Mwanza na sehemu nyingine nyingi.Kwahiyo watu wataniona tu kwenye jukwaa hivi karibuni”.Alisema

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging