Google PlusRSS FeedEmail

P THE MC NA GRAFFITI EVENT

Graffiti event ni tamasha lilifanyika jumamosi ya tarehe 21 pale Nafasi Arts Mikocheni.Tamasha hilo ambalo liliusisha sanaa ya uchoraji pamoja na muziki wa hiphop,ambapo walioudhuria walipata nafasi ya kuona mengi katika uchoraji pia katika swala zima la music wa hiphop.

HNH ni moja kati ya watu walikuwepo katika tamasha hilo,inaweza kuwa jina likawa geni katika masikio yako lakini ni moja kati ya wasanii wachache walipanda na kutoa freestyle na kupelekea kushangiliwa zaidi na mashabiki waliokuwa wameudhuria tamasha hilo.

Wasanii wengine walikokuwepo ni pamoja na Fid q,Nikki Mbishi,Mkoloni wa Wagosi wa kaya,Tifa Flow na wengine wengi.

Katika tamasha hilo la Graffiti event watu walipata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuchora bila gharama yoyote ile,Na baadae kupata burudani kutoka kwa wakali P the mc,Zaiid na mkali Stosh.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging