Google PlusRSS FeedEmail

JOHN MAKINI KUJIGHARAMIA KIMATAIFA

MwanaHipHop maarufu nchini ‘Joh Makini” ambaye amekuwa gumzo baada ya kuachia video yake ya don’t bother,amesema analazimika kutumia gharama kubwa katika video zake anazofanya,ili azidi kujitangaza kwenye soko la muziki kimataifa.

Joh Makini alisema kwa sasa ameshafika hatua ya kimataifa,hivyo ni lazima afanye video zenye hadhi ya kimataifa.

Kwa hatua ambazo naenda natakiwa kulipa fedha kubwa katika video,gharama ya don’t bother ni zaidi ya Tsh milioni 20.7,hapo hauja ongezea manunuzi ya mavazi na vingine.

Joh amesema video hiyo imemfanya kuvunja rekodi ya video zote alizofanya na kuzidi kumtengenezea njia nzuri.

Pamoja na hayo,Joh Makini ameizungumzia kolabo yake na Davido ambayo inatarajiwa kutoka siku za hivi karibuni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging