Google PlusRSS FeedEmail

NIKKI WA PILI AWATAKA WASANII KUPELEKA NYIMBO ZAO NDANI YA RADIO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nikki wa Pili ameweka wazi kuwa msanii mpya kwenye gemu la muziki nchini ananafasi ya kufanya vizuri kuliko msanii aliyekuwa na miaka mingi kwenye gemu hilo.

Aliyazungumza hayo wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Baba Swalehe katika kipindi cha The Jump Off  ya Times Fm radio Nikki alisema,  “kwangu naona ni rahisi msanii mpya kufanya vizuri kuliko msanii aliyekuwa kwenye game kwa miaka mingi."

Unaona kama Chemecal vile unajua ukishakuwa kwenye game kwa miaka mingi kuna ugumu maana watu wanakuwa wamekuzoe.Hivyo inabidi ukaze zaidi ila ni rahisi zaidi kwa msanii mchanga.

Hata hivyo Nikki aliwaasa wasanii wenzake ambao sasa wanaachia tu nyimbo katika social media na kuwataka wapeleke radio maana watanzania walio wengi hawana uwezo wa kupakua nyimbo hizo kwa changamoto nyingi,ikiwemo mtandao.Lakini radio inafika mahali pakubwa zaidi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging