Jumatano ya November 4 ilikuwa ni birthday ya Sean John Combs maarufu kama Diddy ambaye amefikisha miaka 46. Katika kusheherekea birthday yake, rapper huyo mkongwe aliamua kuwa-surprise mashabiki wake kwa kuachia mixtape mpya ‘MMM’ (Money Making Mitch) ambayo ameitoa bure kwa yeyote anayetaka kudownload.