Google PlusRSS FeedEmail

SELFIE YAMPAISHA KOFFIE OLOMIDE

                               

Koffie Olomide amerudi tena kwenye chati za muziki barani Afrika tangu aachie wimbo wake mpya, Selfie katikati ya mwezi uliopita.

Kama unasikiliza redio na kutazama TV za Tanzania utakubaliana nasi kuwa wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo zinazochezwa zaidi kwa sasa.

Selfie unafanya vizuri katika bara lote la Afrika na nchi za Ulaya zikiwemo Ufaransa, Ubelgiji na Canada na umeweza kuwavutia mashabiki wengi vijana tofauti na nyimbo zake za hivi karibuni.

Mastaa akiwemo Didier Drogba wameshapost video kwenye mitandao ya kijamii wakichukua selfie huku wakisikiliza wimbo huo.

Wimbo huo unapatikana kwenye album yake mpya iitwayo ‘13th Apostle’ iliyozinduliwa mwezi uliopita. Hiyo ni album yake ya 20.

Akiongea na BBC hivi karibuni, muimbaji huyo amedai kuwa muziki wake wa sasa utawalenga zaidi vijana. Alisema kuwa kupitia lebo yake, ‘Koffi Central’ atasimamia wasanii wachanga, kutengeneza na kutunga nyimbo kwaajili ya watu wengine.

Katika mahojiano hayo pia Koffi Olomide alizungumzia ukweli kuwa muziki wa Nigeria kwa sasa ndio unaosikilizwa zaidi kuliko wa nchi zingine.

Alisema kuwa ni kweli muziki wa Congo ulijikuta umepitwa lakini kwa nyimbo kama Selfie na zingine muziki wao unaanza kurudi tena kwenye chati. Alisema kuwa muziki wa Congo hauna wadhamini lakini wanamuziki wameendelea kupambana. Alisema hakuna anayebisha kuwa muziki wa Congo ulifungua njia za muziki mwingine Afrika.

Katika hatua nyingine Koffi alijisifia kuwa anajiona kuja kuwa Rais wa Afrika. Alisema kuwa baada ya kuacha muziki anatamani kuja kuwa ‘Rais wa Afrika’.

“Kama siku moja atachaguliwa kiongozi mkuu wa Afrika, nitakuwa mgombea, sina mafunzo ya siasa, lakini nataka niwe rais huyo wa Afrika.

Alisisitiza kuwa angependa siku moja kuona Afrika inakuwa ni nchi moja.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging