Google PlusRSS FeedEmail

JUMA KASSIMU KIROBOTO ATISHIWA BASTOLA

Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’ amefyatuliwa risasi katika tukio la ugomvi Mtu ambaye anadaiwa kumfyatulia Nature risasi hajafahamika lakini inadaiwa ni mtu wake wa karibu waliyetibuana katika mazingira ya ‘kula bata’.
Awali vyanzo vyetu vilidai kwamba wawili hao, walitibuana wakiwa kwenye klabu moja iliyopo Temeke, Dar es Salaam Alhamisi iliyopita.
Hata hivyo, chanzo kingine kilidai kwamba Nature alitibuana na jamaa yake huyo mtaani kwao Temeke.
“Jamaa alifyatua risasi lakini alipiga juu, hakumlenga Nature. Unajua ilikuwa ni ugomvi mkubwa, kwa hiyo Nature baada ya kusikia milio ya risasi alilala chini kwa sababu aliamini anampiga yeye,” kilisema chanzo chetu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging