GADNA KUSABABISHA REDD'S MISS ILALA LEO
Wasanii nguli wa kizazi kipya pamoja na Machozi band leo watayapamba mashindano ya kumsaka ‘Malikia wa Ilala’ Redd’s Miss Ilala 2012, yatakayofanyika kesho Nyumbani Lounge Dar es Salaam
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mratibu wa mashindano hayo Gadna G Habash ilielezwa kuwa licha ya wasanii hao MC katika kinyang’anyiro hicho atakuwa msanii anayeigiza sauti za viongozi mbalimbali nchini maarufu Steven Nyerere
Alisema mwaka huu Ilala inatarajia kutetea taji lake linaloshikiliwa na Salha Israel ambaye ni Miss Tanzania 2011 kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya