MASHUJAA KUONESHA MAVAZI
Bendi ya muziki wa dansi nchini ya Mashujaa , Wanakibega inatarajia kufanya onesho la mavazi ya kizamani katika ukumbi wa Business Park Septemba 15 mwaka huu
Katika onesho hilo litakalowashirikisha wazee ambao ndio watakaokuwa majaji wataongozwa na wanamuziki mkongwe Kassim Mapili na Masoud Masoud
Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema mshindi wa kwanza katika onesho hilo atazawadiwa simu ya mkononi pamoja na fedha taslimu.Sospeter alisema katika onesho hilo mtangazaji nguli nchini Julius Nyaisanga ndiyo atakuwa mshereheshaji
Pamoja na hayo alisema kuwa Wanakibega wataendelea na ratiba yao ya kila wiki ambapo Jumatano watakuwa Sunsent Club Yombo