Google PlusRSS FeedEmail

OMMY DIMPOZI KUZINDUA BAADAE VIDEO MWISHONI MWA WIKI HII

Mwanamuziki wa muziki wa Kizazi kipya anaetamba na nyimbo zake mbili za Nai Nai na Badaye, na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Ommy Dimpoz anataraji kuzindua Video yake mpya ya Baadaye katika ukumbi wa Club Maisha Septemba 9, 2012 jijini Dar es Salaam.Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika na ya kuvutia.Mubenga amesema Ommy Dimpoz ameifanyia shooting video yake hiyo nchini Afrika Kusini.Aidha Mubenga amesema kuwa kazi ya utayarishaji wa video hiyo ilifanywa na Adam Juma wa Visual Lab ambaye ndiye walisafiri nae hadi Afrika Kusini na wameshoot kwenye maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.“Kazi hii ni ya uhakika ambayo tunaizidua Jumapili hii na Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton na nikatika location kali na za uhakika,”alisema Mubenga. Amesema wasanii kadhaa watasindikiza uzinduzi huo akiwepo Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3 siku hiyo katika uzinduzi wa video hiyo mpya na Dimpoz nae atakuwa katika muonekano tofauti si Dimpoz waliyemzoea.Pia Meneja huyo wa Omy Dimpoz amesema akiwa nchini Afrika kusini Dimpoz alimshirikisha Model ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi wakali wa Muziki nchini humo anaejulikana kwa jina la Tully Tshabalala. “Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva wakae tayari kwa video hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya Televisheni nchini na kumbi za burudani baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging