KESI YA LL COOL J KUUNGURUMA SEPTEMBA 10
Mtu aliyevaamia nyumba ya rapa mkongwe LL Cool J ameonekana hana hatia katika tukio hilo na kuachiwa huru na Mahakama kabla ya kukamatwa tena
Jonathan A. Kirby 56, ambaye alifanya tukio hilo alishawahi kufungwa jela kesi yake hiyo imepangwa kusikilizwa September 10 huko Los Angeles. Kirby, amekuwa ni mzululaji ambaye hana kazi na polisi walimpeleka katika hospitali moja ya watu wenye ugonjwa wa akili kwa ajili ya kupima afya yake
Kirby alikamatwa Agosti 22 baada ya polisi kupigiwa simu kutoka katika nyumba ya LL Cool J na mtoto wa Jamess Todd Smith baada ya kugundua yupo nyumbani kwake Los Angeles