Google PlusRSS FeedEmail

KING MAJUTO KUSTAAFU KUIGIZA

Mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu Nchini Amri Athuman ‘King Majuto’ amesema kuwa ifikapo mwezi wa 11 mwaka huu itakuwa ndio mwisho wake wa kuigiza na hataigiza tena , bali jambo atalofanya ni kuwaongoza wanaye na wasanii wengine wanaoigiza na kuchekesha.“Umri wangu umekwenda sana kwa hiyo sioni kama ni sawa kung’ang’ania kuigiza, lakini jambo lingine wachekeshaji wa Tanzania hatuna thamani kazi zetu hakuna anayezijali na kuzipa thamani kama wenzetu wa nje, hiyo sasa si kazi bora nikavue samaki au nilime, unapatana na msambazaji bei nzuri anakuja mwingine anasema kazi yake anauza bei ya chini kabisa sasa bora kufanya kazi nyingine,”anasema King Majuto.Majuto aliyasema hayo baada ya mtayarishaji mmoja kudai kuwa wasanii wanaocheza Komedi hawana gharama baada ya kuigiza katika Komedi yake na gharama yake kuwa ni laki nane za Kitanzania, huku yeye akilipwa zaidi ya milioni tatu hadi nne kwa kuigiza tu, King Majuto anasema kuwa wasanii wa filamu wanalipwa fedha kidogo kwa sababu wanajitambua na kuichukulia kuwa ni kazi rasmi na si mchezo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging