PANDU KUNOGESHA USIKU WA SAUTI
Mwimbaji nyota nchini ambaye aliwahi kutamba na bendi mbalimbali za muziki wa dansi , Mhina Panduka ‘Toto Tundu’ anatarajia kuwepo kwenye onesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa kweli litakalofanyika baadaye mwezi huu
Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa Endless Fame , Zulfa Msuya alisema Mhina ni mmoja kati ya wanamuziki watakaoungana na Ibonda Katumbi ‘ Jesus’ na Diamond Sound katika usiku huo
“Kama tulivyosema awali wapo wanamuziki wengi maarufu ambao watashiriki kwenye usiku huu, Pandu atakuwepo pale kwa ajili ya kuimba nyimbo zake maarufu kama kulala sebuleni , pole Mama James ,You still Mine na kesho kwa mungu” alisema
Pandu ambaye kwa sasa yuko na kundi la TOT, amewahi kupigia bendi kadhaa maarufu nchini zikiwemo Mwenge Jazz ambayo ndoyo ilimtambulisha kwenye ulimwengu wa muziki baada ya nyimbo mbili alizoimba kufanya vizuri katika miaka ya 1980