Wema na Prezoo walikutana katika shoo ya Serengeti Fiesta ya mjini Moshi na Tanga na wawili hao kudaiwa kukutana pamoja na kuzungumza kwa masaa kadhaa , habari kutoka kwa mtu wa karibu na Prezoo zinasema kuwa Wema na Prezoo walifanya mazungumzo kwa muda mrefu kiasi cha kushangaza wengi wanaomfahamu mwanadada huyo
Wema kwa sasa hanauhusiano unaofahamika hasa baada ya kuachana na msanii wa Bongo fleva Diamond mmoja wa wasanii nyota wanaotamba nchini
“Yule dada amekuwa karibu na Prezoo kwa masaa kadhaa mara baada ya kukutana Moshi na jijini Tanga,hivyo huenda kuna jambo la siri linaloficha na wasanii hao ambao wote wana majina makubwa
“Nilimuona Wema na Prezoo wamejifungia ndani kwa masaa kadhaa ingawa sijajua ukaribu huo wa ghafla walikuwa wanazungumzia mambo gani mahali penye utulivu huo baada ya shoo ya fiesta “ alisema mtoa habari huyo
Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii maarufu mno jambo linalomfanya afuatiliwe kwa karibu na wadau wa filamu hapa nchini