AKUDO YAMREJESHA MNENGUAJI WAKE
Bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact imemrejesha kundini mnenguaji wake wa zamani Nataly Mbuyi aliyetimulia kwa utovu wa nidhamu na kukaa nje ya bendi hiyo zaidi ya miezi mitano
Akizungumzia swala hilo la kumrejesha mnenguaji huyo Meneja Uhusiano wa bendi hiyo, Ramadhani Pesambili alisema kuwa mnenguaji huyo alirejeshwa wiki iliyopita ili kuendelea na kazi katika bendi hiyo inayoitwa 'Vijana wa Masauti'
"Alikuwa amekimbilia kwenye bendi ya Mashujaa Musica lakini yakamshinda na kuamua kurudi Akudo nasi tumempokea kwani tunaamini kwamba atakuwa amejifunza mengi" alisema