FILAMU YA BODABODA KUTOA SOMO KWA MADEREVA
Kampuni ya Genius Entertainment imekamilisha filamu ya Bodaboda Killers yenye lengo la kutoa elimu na ushauri kwa serikali, madereva wa pikipiki 'bodaboda' jinsi ya kukomesha na kudhibiti uporaji na mauaji ya madereva hao itakayotoka muda wowote kuanzia sasa
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni mmoja wa kiongozi wa kampuni hiyo ambaye pia ndiye Mtunzi wa filamu hiyo, Adarusi Walii alisema filamu hiyo imebeba matukio mbalimbali ambayo hufanyiwa madereva wa bodaboda na jinsi ya kutatua matatizo hayo
Alisema madereva hao hukumbwa na mikasa mbalimbali kama kutekwa kuuwawa na kujeruhiwa kutokana na sababu mbalimbali hivyo anaimani kuwa filamu hiyo itakapotoka itakuwa soko kwa watu wote
Aliwataja baadhi ya wasanii maarufu nchini ambao wameshiriki katika filamu hiyo kuwa ni Kulwa Kikumba 'Dude', Chuchu Hans, Biso na Biso na muimbaji wa Jahazi, Prince Amigo na wengine wanaochipukia kama Zena na Nguzo