Google PlusRSS FeedEmail

RAYUU: NIMECHORA TATOO KWA AJILI YA MPENZI WANGU


Msanii anayekuja juu katika tasnia ya filamu na tamthilia nchini Alice Bagenzi 'Rayuu' amezidi kujichora tatoo kwenye mwili wake ambapo sasa amevuka mipaka na kujichora kiunoni na sehemu nyingine nyeti

Alipotafuta msanii huyo na baada ya kupatikana alidai kuwa amejichora tatoo nyingi ndani ya mwili wake na hazina ubaya wowote

Rayuu alipobanwa zaidi na maswali kuwa amechora kwa maana gani alidai kuwa tangu alipokuwa mtoto alipenda sana kujichora mwili wake na kwa sasa anaona zitakuwa na maana kama urembo ndani ya mwili wake lakini zipo nyingine atazitumia kama zawadi kwa mpenzi wake ingawa bado hajampta yule mwenye mapenzi ya dhati

"Tatoo nimechora na lakini wapo ambao wanakuza mambo na kunifanya nishindwe kunywa hata maji kwa kudai kuwa nimechezea mwili wangu wakati vitu ninavyovifanya hakuna mtu anayenipa ushauri zaidi ya nafsi yangu inavyonituma" alisema


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging