Google PlusRSS FeedEmail

BEN AFFLECK AGONGA GARI NA KUACHA UJUMBE



Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa nchini Marekani Ben Affleck amepata ajali ndogo ambayo imekuwa gumzo nchini humo. Ben akiwa na gari lake aina ya Honda aligonga gari nyingine ambalo ilikuwa limeegeshwa na kuvunja kioo cha upande wa nyuma

Kutokana na hali hiyo Ben aliamua kushuka na kumtafuta mwenye gari hilo lakini jitihada zake ziligonga mwamba , hali hiyo ilimlazimu Ben kuacha ujumbe kwenye gari hilo kuwa "nimegonga gari lako na kuvunja kioo kwa bahati mbaya nambar zangu za simu zipo hapo naomba unitafute"

Hali hiyo ya kiungwana ndio imefanya tukio hilo kuwa gumzo kwani kwa mazingira ya kawaida alikuwa anaweza kuondoka bila kujali chochote

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging