Mwanamitindo maarufu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwengelo amezindua rasmi kampuni ya Kidoti, Dar es Salaam itakayokuwa na lebo ya kidoti kwa ajili ya masuala ya mitindo na urembo
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam ambao ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa urembo, maonyesho ya mavazi,wanamitindo na wauzaji wa bidhaa hizo, Jokate alisema rebo hiyo ilianza kujihusisha na maswala ya mitindo mwaka jana ambapo hatua ya kuanzisha ni moja ya mikakati ya kujitafutia fedha kama mjasiriamali na lengo kubwa ni kutaka kusimama yeye mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu
Alisema mbali ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali, pia atakuwa anasambaza bidhaa za kampuni hiyo ambazo ni nywele na nguo kwenye maduka ili kuwawezesha wananchi kutumia bidhaa zake
"Lengo langu kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea hiyo ndio ndoto yangu pamoja na kuhakikisha fani hiyo ya urembo na mitindo inakuwa na muonekano tofauti ikilinganishwa na ilivyo hivi sasa " alisema