Google PlusRSS FeedEmail

CHRISTINA MILIAN AMSIFU BOSI WAKE LIL'WAYNE



Tangu aliposaini mkataba wa kufanya kazi chini ya lebo ya Young Money, Christina Milian amekuwa studio akiandaa albamu mpya

Muimbaji huyo wa kibao cha 'Dip It Low' alihudhuria kipindi cha 'Big Boys Neighborhood'cha radio Power 106 kuzungumzia kazi yake mpya chini ya lebo ya YMCMB na mambo yaliyo chini ya bosi wake mpya Lil Wayne

"Wayne anasaidia sana wasanii wake, jambo ambalo ni kubwa sana" alisema "Nina mahusiano moja kwa moja ya kikazi na kila mtu kuanzia Mack (Maine)hadi Wayne, wahusika kila hatua huchangia muziki kucheza nyimbo na kuiwekea vionjo vyao

Christina amejiandaa kuachia single yake mpya na video hivi karibuni "nataka kuchagua nyimbo sahihi wa kutoa hata hivyo". Christina ambaye albamu yake ya mwisho iliyoitwa 'So Amazin'ilitoka mwaka 2006 "Ni muda mrefu tangu niwe njee ya muziki hivyo sitaki kushindwa na siamini kwenye kushindwa hivyo najaribu mambo mapya na kuweka mambo hayo pamoja"

Hilo ndio jambo moja kubwa la Wayne, huwa anasisitiza 'fanya kazi na maproduza tofauti, fanya taratibu lakini wakati huo huo jaribu mambo mapya usikomalie jambo moja tu

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging