CISSY: BOBBI KRISTINA ATAKUFA MAPEMA
Cissy Houston ambaye ni mama mzazi wa marehemu Whitney Houston, anahofia mjukuu wake Bobbi Kristina huenda akafariki mapema kutokana na kubobea kwenye matumizi ya dawa za kulevya
Zaidi ya hilo, Cissy amedokeza kuwa sababu nyingine inayoweza kufupisha uhai wa mjukuu wake, ni binti huyo kupata kiwewe juu ya wingi wa fedha alizoachiwa na marehemu mama yake
Akizungumza na TMZ, Cissy alisema Bobbi amekuwa pia akichanganywa na vitu vingi ikiwemo mpenzi wake NiCK Gordon na baba yake Bobby Brown
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kinasema kuwa Cissy amekuwa akihitaji kijana huyo kupewa fedha za mama yake pindi atakapokuwa mtu mzima zaidi kuliko hivi sasa ambapo ana umri wa miaka 19
Alisema kija huyo hatakiwi kupewa kiasi cha fedha alichoacha mama yake kama ilivyoshauliwa na mahakama kiasi cha dola milioni 20