RECHO KUWAPELEKEA KIZUNGUZUNGU MASHABIKI WAKE KATIKA STAGE YA CLUB BILICANAS JUMAPILI
Ni jumapili nyingine ya burudani ndani ya Club Bilicanas ambapo mwanadada anayetamba na kuja juu kwa kasi ya ajabu katika tasnia ya muziki, ambaye ni mmoja wa wasanii wanaotoka katika nyumba ya kukuza vipaji THT Rachael Haule 'Recho' anatarajia kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wake ndani ya club hiyo siku ya tarehe 14 mwezi huu
Mwanadada huyo mwenye uwezo wa kumiliki stage huku akiwaacha mashabiki wake hoi kwa uwezo wake alionao wa kuzungusha nyonga huku akienda sambamba na mapigo ya nyimbo zake, msanii huyo anatamba na ngoma kibao kali ikiwemo Nashukuru, Upepo pamoja na Kizunguzungu,